Zaidi ya familia 141 zimelazimika kuyahama makaazi yao katika wilaya ya mjini Unguja kutokana na kuingia na maji yatokanayo ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo mbali mbali na kusababisha baadhi ya familia kulazimika kuhama makaazi yao.
Baadhi ya maeneo yalioathiriwa na mvua hizo ni shehia ya mwanakwerekwe mjini Unguja,tomondo ,ziwa maboga,ziwatuwe,pangawe,kinuni na baadhi ya maeneo mengine mbali mbali.
Baadhi ya wahanga wa kadhia hio wakizungumza na gazeti hili walisema wamelazimika kuhama kwa sababu ya uwepo wa mvua kubwa zaidi usiku wa kuamkia jana.
Juma Abdalla Kheri mkaazi wa Tomondo alisema imemlazimu kuhama baada ya maji mengi kuingia kwneye nyumba yake kupitia sehemu mbali mbali na kufanya nyumba hio kujaa maji.
Alisema kwa sababu ya mazingira hayo alilazimika kuhamisha baadhi ya vitu vyake ndani ya nyumba hio usiku wa manane na kusema bila ya kufanya hivyo hwenda madhara makubwa zaidi yangemtokea.
Asya Awadhi wa ziwamaboga alisema hadi sasa bado hana sehemu maalumu ya kukaa badala yake imemlazimu kuomba shemu ndogo kwa majirani zake kutokana na tatizo kama hilo ambalo limewakumba wengi.
Marina Joel Thomas alisema ipo haja ya wananchi kuwa makini zaidi katika kipindi hichi na kuwataka kuhama katika maeneo yaliohatarishi na mvua hizo.
Alisema jamii inapaswa kujikinga na athari hizo ambazo hwenda zinaweza kuwa kubwa zaidi iwapo wataendelea kubakia katika maeneo yote yalio hatarishi.
‘’Mvua hizi zimeanza hatujui itakuaje hapo badae sasa natoa raia wananchi wote wahame kwenye maeneo hatarishi na wasisubiri maafa zaidi ambayo yanaweza kuwakumba’’aliongezea.
Naibu Mkurugenzi kamisheni ya kukabiliana na maafa Zanziabr Muhidini Ali Muhidini alisema kwa kiasi kikubwa wananchi wamehamaisika kuhama kwenye maeneo hatarishi.
Alisema hali hio imediriki kutokana na elimu waliopatiw akutoka katika kamisheni hio ya kukabiliana na maafa na kwamba utaratibu huo hwenda ukawanusuru wengi kuepuka na majanga zaidi.
Hata hivyo alisema kukubali huko kwa jamii kuhama kwenye maeneo hayo kunaipunguzia mzigo Serikali ambao ungeweza kujitokeza vifo na mengineyo.
Pamoja na hayo aliseka kamisheni hio ipo karibu na wananchi zaidi katika kipindi hichi na imejiandaa na lolote lile ambalo litatokea.
0 Comments