Windows

Msuva avunja rekodi yake



MSHAMBULIAJI wa Difaa El Jadida ya Morocco, Saimon Msuva amevunja rekodi yake ya mabao 11 ya msimu uliopita wa Ligi Kuu Morocco ‘Batola Pro’.


Kabla ya mchezo wa jana kati ya Difaa na Youssoufia Berrechid, Msuva alikuwa na mabao 12 ambayo aliyafikia wiki iliyopita ambapo alifunga mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Moghreb Tetouan.


Akizungumzia kuvunja kwa rekodi yake ya msimu uliopita, Msuva alisema ni kitu ambacho alikitarajia hivyo anachokitazama mbele ni kufikia malengo yake ya msimu huu.


Msuva alisema msimu huu, alijiwekea malengo ya kuwa mfungaji bora wa Batola Pro ambayo imesaliwa na michezo kadhaa kabla ya kumalizika.


“Kuna mechi tatu mbele yetu hadi nne kwa wengine zimebaki, nina muda wa kupigania ufungaji bora katika michezo hiyo maana ukiangalia nimezidiwa mabao matano na anayeongoza.


“Nikiwa mfungaji bora yatakuwa mafanikio makubwa kwangu kuliko kuvunja rekodi yangu ya msimu uliopita,” alisema Msuva.


Mtogo Laba Kodjo wa Berkane ndiye mshambuliaji anayeongoza katika orodha ya mastaa kwenye Batola Pro wanaowania Kiatu cha Dhahabu akiwa na mabao 17.


Post a Comment

0 Comments