Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema lengo la kwanza la kikosi chake msimu ujao ni kutwaa ubingwa wa ligi kuu
Yanga imeshindwa katika mbio za kuwania ubingwa msimu huu na wapinzani wao Simba ambao wanahitaji alama moja tu kutoka michezo mitatu
Hata hivyo licha ya kumaliza katika nafasi ya pili, Zahera amesema timu yake imefanikiwa kulingana na mazingirwa waliyokuwa nayo
"Tulianza kwa kuwa na malengo ya kumaliza nafasi ya sita au saba, lakini baada ya kuona tunafanya vizuri licha ya kuwa na changamoto nyingi, tukasema tujaribu kuwania ubingwa," amesema Zahera
"Bado naamini tulistahili kushinda kombe kama sio kudhurumiwa baadhi ya michezo"
"Sasa nafurahi timu imepata viongozi, nimewaambia wajipange. Hatutaki tena haya ya mwaka huu yatukute msimu ujao"
"Tunahitaji kuwa na timu imara itakayoshinda na kutwaa ubingwa mapema"
Zahera amesema huu ukiwa msimu wake wa kwanza Tanzania, umemsaidia kufahamu ushindani wa ligi, aina ya wachezaji anaowahitaji na mbinu gani atumie ili kuweza kufanya vizuri
"Tutatengeneza timu imara, tutasajili wachezaji wa kiwango cha juu ambao watafanya timu yetu iwe kali sana msimu ujao
0 Comments