Windows

Mechi tano za ubingwa Simba


Kikosi cha Simba kimerejea jijini Dar es salaam jana kikitokea mkoani Mbeya ambako kilifanikiwa kushinda michezo yote miwili dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons
Simba inajiandaa kucheza na Coastal Union kesho kwenye mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru
Baada ya kucheza takribani michezo saba nje ya jiji la Dar es salaam, Simba imerejea Dar ambapo ratiba inaonyesha itacheza michezo mitano mfululizo kabla ya kutoka tena kumalizia michezo miwili
Mchezo dhidi ya Coastal Union ni kwanza kati ya michezo hiyo, ambapo pia itazihusu Kagera Sugar (10/05), Azam (13/05), Mtibwa (16/05) na Ndanda Fc (19/05)
Kimahesabu, kama Simba itashinda michezo yote mitano, basi itatwaa ubingwa mapema tu bila ya kujali matokeo ya michezo mingine mitatu
Yanga yenye alama 80 inaweza kufikisha alama 92 kama itashinda michezo minne wakati Simba ikishinda michezo hii mitano itafikisha alama 93

Post a Comment

0 Comments