Mshereheshaji, Emanuel Mathias (34) maarufu kama MC Pili Pili na mwenzake wameachiwa kwa dhamana katika kesi ya kuchapisha maudhui katika mtandao bila kuwa na leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ( TCRA)
Mbali na Mathias, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Heriel Clemence( 25) ambapo wamesomewa mashitaka yao na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando.
Mbali na Mathias, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Heriel Clemence( 25) ambapo wamesomewa mashitaka yao na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando.
Wakili wa Serikali, Constantine Kakula alidai wakati akisoma hati ya mashtaka leo Mei 7, 2019, kuwa wawili hao walitenda kosa hilo kati ya Novemba 17, 2013 na Mei 2, 2019 wakiwa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Kakula, ambaye alisaidiana na Batilda Mushi, alidai mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama hiyo, Augustina Mmbando kuwa katika kipindi hicho, MC Pilipili na Clement walichapisha maudhui kwa kutumia televisheni ya mtandaoni (online TV) inayojulikana kwa jina Mc Pilipili, bila kuwa na kibali cha TCRA.
Washtakiwa baada ya kusomewa shtaka lao, walikana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika ambapo wakili wa utetezi Jebrah Kambole aliwaombea dhamana washitakiwa hao.
MC Pilipili na Clemence wameachiwa huru kwa masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua kutoka kwa Mtendaji wa Kata na barua ambayo imepitishwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa, anakotokea mdhamini huyo.Kesi imeahirishwa hadi Mei 7, 2019.
0 Comments