Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akisisitiza jambo wakati akiongoza kikao cha Bunge la Afrika leo Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.
***Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuchukua hatua za haraka kusaidia nchi za Kusini mwa Afrika (Msumbiji,Malawi na Zimbabwe) zilizoathirika na Kimbunga cha Idai.
Mheshimiwa Masele ambaye pia ni Mbunge wa Shinyanga Mjini ametoa pongezi hizo leo Mei 7,2019 akiongoza kikao cha Bunge la Afrika kinachofanyika Jijini Johannesburg,nchini Afrika Kusini wakati wabunge wakijadili kuhusu Ripoti ya kazi ya Umoja wa Afrika (AU).
Mhe. Masele alilazimika kutoa ufafanuzi baada ya hoja kuibuka hoja bungeni kuwa nchi za Umoja wa Afrika zimekuwa hazichukui hatua za haraka panapotokea majanga mbalimbali.
“Nitumie fursa hii kuipongeza sana serikali inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kwa kuchukua hatua za haraka kusaidia chakula na madawa kwa nchi zilizokumbwa na Kimbunga Idai”,alisema Mhe. Masele.
“Serikali ya Tanzania ilikuwa mstari mbele kutoa msaada wa chakula,dawa na vifaa vya kujiihifadhi kwa nchi ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika”,aliongeza Mhe. Masele.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akiongoza kikao cha Bunge la Afrika leo Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akiongoza kikao cha Bunge la Afrika leo Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini. Katikati ni Rais wa Bunge la Afrika, Mhe. Roger Nkodo Dang akitoa taarifa ya kazi ya Bunge la Afrika.
Wabunge wakiwa ukumbini.
0 Comments