Windows

Maoni ya Yondani kuhusu maboresho ya kikosi cha Yanga


Nahodha wa zamani wa Yanga Kelvin Yondani 'Vidic' ametoa maoni yake juu ya nini kifanyike kuifanya Yanga iwe bora msimu ujao
Yondani mchezaji mwandamizi zaidi katika kikosi cha Yanga amesema licha ya kupambana msimu huu, walikuwa na changamoto kadhaa zilizowafanya washindwe kufikia malengo yao
"Timu yetu inahitaji maboresho madogo ya kikosi kwa kuanza ni kusajili washambuliaji wa kati, mabeki wa kati na kipa ambao wote wenye uzoefu wa kuamua mechi"
"Ukiangalia hivi sasa katika timu mshambuliaji tunayemtegemea ni mmoja pekee ambaye ni Makambo, kama siku ikitokea akawekea ulinzi mkali, basi timu inakuwa ni vigumu kupata matokeo, hivyo ni lazima tusajili washambuliaji kama kweli tunataka ubingwa msimu ujao," Yondani alisema katika mahojiano na Sport Xtra
"Pia, kipa anahitajika yule mwenye uwezo na uzoefu kwa sababu kama mabeki wakiwa wazuri halafu kipa akawa hana uwezo ni lazima tutafungwa"
Aidha, Yondani anaamini safu ya kiungo ya timu hiyo iko imara na hadhani kama kuna ulazima wa kuifanyia mabadiliko
"Safu ya kiungo binafsi naona hakuna haja kusajili wengine kwani tayari wapo Fei Toto , Banka, Bobani na Tshishimbi wote wapo vizuri"
Yanga iko kwenye mchakato wa kuboresha kikosi chake ambapo inaelezwa timu hiyo itafanyiwa mabadiliko makubwa kulingana na maoni ya kocha Mwinyi Zahera kwa uongozi mpya wa timu hiyo
Uongozi wa Yanga chini ya Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla umesema utampatia Zahera fedha alizoomba (Bil 1.5 au zaidi) ili kuhakikisha anatengeneza timu imara itakayoakisi hadhi na sifa ya Yanga

Post a Comment

0 Comments