Windows

MAKAMU MWENYEKITI YANGA ALIVYOZUNGUMZIA KIPIGO CHA LIPULI FC



Yanga wanadai kupoteza dhidi ya Lipuli FC ya Iringa katika mchezo wa FA, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)  ndio chanzo kutokana na kukataa kubadilisha ratiba.
 Yanga ilipokea kipigo cha mabao  2 -0 dhidi ya Lipuli katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Samora, Iringa katika mchezo wa FA.


Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa, kuwepo kwa mambo mawili katika klabu yao ndio kumewagharimu kuweza kupoteza mchezo huo.
“Kitu kilichotugharimu kupoteza mchezo na Lipuli ni kuwa na mambo makubwa mawili kwa wakati mmoja ikiwemo lile la uchaguzi na hili la mchezo wetu wa FA ambao hatukuweza kufanya maandalizi mazuri kutokana na uchaguzi.


“Tuliwaomba TFF waweze kusogeza mbele mchezo huu lakini walitukatalia hivyo matokeo yamekuwa haya na Wanayanga wote wamekubaliana na matokeo hivyo tunajipanga zaidi kwa ajili ya msimu ujao.


“Tunahitaji kukamilisha mechi zetu za ligi zilizobakia kwa kuhakiksha tunashinda huku tukijipanga kwa ajili ya msimu ujao,” alisema Mwakalebela ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa TFF na kuongeza:


“Unapokuwa na mambo makubwa mawili mazito moja lazima litakuzidi  nguvu, ilitumika nguvu zaidi kwenye uchaguzi,” aliongeza.



Post a Comment

0 Comments