NI kama straika matata wa Yanga, Heritier Makambo, amebakiza hatua chache tu kabla ya kukamilisha dili la kwenda kukipiga nchini Ubelgiji msimu ujao.
Ndio, yule bosi wa klabu ya Waasland Beveren, ambayo Mwanaspoti lilikueleza kuwa anatua nchini muda wowote ndio amefika kuja kusimamia mazungumzo ya uhamisho wa Makambo.
Juzi, Mwanaspoti toleo la jana Jumanne Mei 21 lilikupa undani ya ujio wa ugeni wa bosi huyo, ni maalumu kwa uhamisho wa Makambo ambaye msimu huu ameifungia Yanga mabao 20 na kati ya hayo 16 akifunga kwenye Ligi Kuu Bara na manne kwenye Kombe la FA.
Aliyetua jana ni Raoul Alfred, raia wa Ubelgiji anayeishi nchini Ufaransa, na amelieleza Mwanaspoti kila kitu kuhusiana na ujio wake nchini.
Raoul alitua nchini jana mchana na kupokewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Omary Kaaya akitokea Ufaransa kuja kukutana mezani na mabosi wa Yanga.
Akizungumza na Mwanaspoti, Raoul alisema ujio wake ni maalum kwa kufungua neema kwa klabu ya Yanga kupitia wachezaji walionao.
\Nafurahi kuwa hapa Tanzania, nimekuja kuonana na kufanya mazungumzo na Yanga ili kuangalia kama tunaweza kuanzisha ushirikiano na mambo mengine baina ya klabu hizi mbili,” alisema Raoul.
Hata hivyo, alisema kuwa jukumu la kwanza lililomleta ni kufanya mazungumzo na Yanga kuhusiana na dili la uhamisho wa Makambo.
“Ndiyo, kuna hilo suala la Makambo namjua ni mchezaji mzuri, ambaye yuko hapa Yanga kwa sasa, lakini ukiacha hilo bado kunaweza kuwa na wachezaji wengine. Hii ni nafasi kwa pande zote,” alisema.
Raoul aliongeza kuwa kazi nzuri inayofanywa na mshambuliaji wa Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta imeivutia klabu ya Waasland na kupitia Mwenyekiti wake Dirk Huyck, kuanza kumulika vipaji vilivyopo Tanzania ila kwa sasa ni Makambo kwanza.
“Najua mnafahamu Samatta anafanya vizuri Ubelgiji, hilo limeifanya Waasland kuangalia fursa zaidi ya wachezaji wanaofanya vizuri hapa Tanzania,” alisema.
Mwanaspoti linafahamu kuwa, kama mazungumzo ya vigogo hao yatakwenda vyema basi Waasland Beveren ipo tayari kuipa Yanga Dola 200,000 (Sh 460 milioni) kwa ajili ya saini ya Makambo, ambaye amebakiza mkataba wa mwaka mmoja pale Jangwani.
KUTIA TIMU UHURU
Taarifa ambazo Mwanaspoti inazo ni kuwa, baada ya mazungumzo hayo Raoul na uongozi wa Yanga ambayo yalipangwa kufanyika jana usiku, basi leo atatua Uwanja wa Uhuru, kumuangalia Makambo na mastaa wengine wa Yanga, wakikipiga dhidi ya Mbeya City.

0 Comments