KITENDO cha straika wa Yanga, Heritier Makambo kusaini mkataba wa awali na Horoya AC, kimeifanya Simba kukosa kiasi cha dola laki tatu (Sh milioni 689) ambazo wangezipata kwa straika wao Meddie Kagere.
Kabla ya kusajiliwa kwa Makambo na Horoya AC ya Guinea, klabu hiyo ilishaweka mezani kiasi cha dola laki tatu kwa ajili ya kumng’oa Simba na Kumpeleka kwenye kikosi chao kwa msimu ujao.
Meneja wa Kagere, Patrick Gakumba Amefunguka, kwamba kabla ya Makambo kusaini mkataba huo, kocha wa kikosi hicho, Didie Gomes alimpigia simu kwa ajili ya kumtaka ampeleke mmoja kati ya mastraika wake Kagere au Jacques Tuyisenge wa Gor Mahia.
“Kabla ya Makambo kusajiliwa Horoya, kocha wao alinipigia simu kwa ajili ya kutaka nimpelekee kati ya Kagere au Tuyisenge na alikuwa tayari ametenga dola laki tatu (milioni 689) kwa ajili ya kumsajili mmoja wao.
“Lakini nikamwambia kwanza aanze na Makambo kwani kwa washambuliaji hao ingekuwa ngumu kidogo, lakini hata hivyo bado anataka washambuliaji wengine wawili na ninaweza kumpelekea baadaye, itategemea na namna nitakavyoelewana na timu zinazowamiliki wachezaji hawa kwa sasa,” alisema Gakumba.
source : Champion

0 Comments