Windows

Ligi Kuu inaisha na utamu wake

PichaPAZIA la Ligi Kuu Bara linatarajiwa kufungwa leo huku mabingwa Simba wakikabidhiwa kombe lao kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa. Lakini utamu hasa wa ligi upo kwenye timu nane za chini, ipi itaungana na African Lyon kushuka daraja na zipi zitacheza ‘play off’.

Awali, Simba ilikuwa ikabidhiwe kombe lake mwishoni mwa wiki iliyopita ilipocheza na Biashara United kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam lakini ilishindikana kutokana na dharura ya mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola. Sasa taji hilo litakabidhiwa leo baada ya mechi dhidi ya Mtibwa Sugar. Kitendo cha uwanja huo kutumika kukabidhi kombe kinajirudia kwani msimu wa mwaka 1999/2000 Mtibwa alikabidhiwa ubingwa hapo alipoifunga Yanga.

Lakini pia kwenye ligi ndogo mwaka 2007 Simba ilikabidhiwa ubingwa hapo ilipoifunga Yanga. Simba inaingia uwanjani leo ikiwa na pointi 92 hivyo mechi ya leo ni ya kulinda heshima zaidi. Hilo pia lipo kwa Mtibwa Sugar kwani hata ikifungwa leo haishuki daraja, hivyo inatafuta kulinda heshima yake isifungwe na Simba mechi zote mbili za msimu huu.

Mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu, wapo nafasi ya tano wakiwa na pointi 49. Nahodha wa Simba, John Bocco amewaita mashabiki wa Simba kuja mjini hapa kuwapa sapoti wakitwaa rasmi kombe lao kwa mara ya pili mfululizo. Mwenyekiti wa matawi ya Simba Dar es Salaam, Oscar Makoye aliliambia gazeti hili jana kuwa wamefanya maandalizi kwa matawi yote ya Dar kujumuika Morogoro na baadhi ya wanachama wao wameanza kuingia tangu jana. Gazeti hili lilishuhudia maandalizi ya mechi hiyo, ikiwa ni pamoja na kubadilisha nyavu za magoli.

Meneja wa uwanja huo John Simkoko alisema wameanza maandalizi mapema, ikiwa ni pamoja na kufyeka majani na kuhakikisha hali ya uwanja iko kwenye usalama. Timu zote 20 zitakuwa kwenye viwanja tofauti leo kukamilisha ratiba zao na wengine kujinusuru na kushuka daraja. Yanga itakuwa Uwanja wa Taifa ikimenyana na Azam, katika mechi nyingine ya kukamilisha ratiba lakini yenye msisimko wa hali ya juu. Mabingwa hao wa kihistoria kwenye Ligi Kuu, wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wakiwa na pointi 86 wakifuatiwa na Azam wenye pointi 72.
Kazi kubwa ya Yanga leo ni kuhakikisha inamaliza ligi kwa heshima huku Azam ikitaka kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza. Kazi kubwa ipo kuanzia Dkwa timu inayoshika nafasi ya 12 Biashara United, JKT Tanzania, Stand United, Mbao FC, Prisons, Kagera Sugar, Ruvu Shooting na Mwadui. African Lyon tayari imeshashuka daraja.

Kwa mujibu wa kanuni za msimu huu, timu mbili za chini zitashuka daraja moja kwa moja na timu zitakazomaliza nafasi ya 17 na 18 zitacheza play off na timu mbili kutoka daraja la kwanza.
Timu hizo nane za chini, ili zivuke ni lazima kila moja ishinde mechi yake,

japo linalozidisha ugumu wa mechi hizo za mwisho. Ruvu Shooting itajitetea dhidi ya Alliance, JKT Tanzania ikicheza
 na Stand United na Mbeya City ikimaliza na Biashara United Uwanja wa Sokoine. Prisons itacheza na Lipuli, African Lyon na KMC, Mwadui na Ndanda na Coastal Union itamaliza na Singida United.

Post a Comment

0 Comments