Rasmi, Manchester United hawatacheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya pointi zao walizokusanya msimu huu kwenye Ligi Kuu England hazitoshi kuwafanya kuingia ndani ya Top Four.
Sare ya 1-1 ugenini kwa Huddersfield imefuta ndoto zao za Man United kumaliza ligi ndani ya Top Four kwa sababu sasa wamekusanya pointi 66 na wamebakiza mchezo mmoja tu, ambao hata wakishinda wataishia kukusanya pointi 69, moja nyuma ya Tottenham waliopo kwenye nafasi ya nne.
Katika mchezo huo uliofanyika jana Jumapili, Man United kwa bao la Scott McTominay kwenye kipindi cha kwanza, lakini Huddersfield walikuja kuchomoa kwenye kipindi cha pili kupitia kwa Isaac Mbenza.
Huddersfield wenyewe wameshashuka daraja, lakini hawataka kuwa wanyonge na hivyo kuwatibulia Man United, ambao sasa msimu ujao watacheza kwenye Europa League tu.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, Chelsea wamepanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya kuibuka na ushindi mtamu kabisa wa 3-0 dhidi ya Watford uwanjani Stamford Bridge.
Mabao ya Ruben Loftus-Cheek, David Luiz na Gonzalo Higuain yalitosha kabisa kukifanya kikosi hicho cha kocha Maurizio Sarri kupanda hadi kwenye nafasi ya tatu baada ya kukusanya pointi 71 ambazo zinawafanya kuwa na uhakika mkubwa wa kumaliza ndani ya Top Four na kupunguzia presha ya kurudi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Wapambanaji wengine wa Top Four ni Arsenal ambao jana usiku walilazimishwa sare 1-1 na Brighton kwenye uwanjani Emirates matokeo hayo ya kikosi hicho cha Unai Emery unafanya vita hiyo ya Nne Bora kusubiri hadi mechi za mwisho kwa timu hizo tatu, Spurs, The Blues na The Gunners.
Kuhusu Man United itabidi wajilaumu tu wenyewe kwa kushindwa kuonyesha njaa ya kusaka ushindi licha ya kugongesha mwamba mara kadhaa huku ikipoteza nafasi kibao za kufunga kwenye mashambulizi yake ambapo ilipiga mashuti saba yaliyolenga goli na kufanikiwa kufunga mara moja tu.
Mchezo mwingine wa ligi hiyo utapigwa leo Jumatatu, ambapo mabingwa watetezi Manchester City watakuwa Etihad kukipiga na Leicester City ya Jamie Vardy.
Man City watashuka uwanjani kwenye mchezo huo wakifahamu wazi kwamba wanahitaji ushindi wa lazima ili kuweka hai matumaini yao ya kuutetea ubingwa huo. Liverpool kwa sasa ndio wanaoongoza ligi baada ya kukusanya pointi 94, mbili zaidi ya Man City.

0 Comments