Windows

Kotei hana muda Simba

 Kiungo Mghana wa Simba, James Kotei ametamba kwa kuwaambia wadau wa kikosi hicho kama kuna mtu analeta za kuleta jibu lake ni moja tu.


Unajua jibu hilo ni lipi? Kotei ambaye wakati mwingine amekuwa mtu wa utani amewaambia wadau wa Simba akitokea mtu wa hivyo jibu lake hatasikilizwa kwa sababu wao wako kileleni mwa Ligi Kuu Bara.


Kotei ambaye anacheza nafasi ya kiungo mkabaji ndani ya kikosi na pacha wake wake ni Jonas Mkude.


"Kama kuna mtu anajaribu kukabiliana na wewe kwa siku ya leo (jana Jumatano) waambie huwezi kuwasikia kwa sababu uko juu kileleni,"alisema Kotei ambaye alisajiliwa pamoja na Mghana mwenzake kipa Daniel Agyei misimu miwili iliyopita lakini mlinda mlango huyo aliondolewa.


Kotei aliitoa kauli hiyo baada ya Simba kuwapiga Coastal Union mabao 8-1 katika mchezo uliopigwa jana Jumatano kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Ushindi huo uliwafanya wakae kileleni mwa Ligi Kuu Bara na kuwapiku watani wao Yanga.


Post a Comment

0 Comments