Windows

Kocha Yanga atamba kuwa na kikosi bora msimu ujao



Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema timu yake inaendelea na mchakato wa kusajili wachezaji wapya watakaorudisha makali ya timu hiyo msimu ujao

Zahera amesema yuko mbioni kukamilisha usajili wa wachezaji nane, akitarajiwa kuweka hadharani majina ya wachezaji hao wiki ijayo

Akizungumza jana, Zahera amesema miongoni mwa wachezaji hao sita wanatoka nje ya nchi na wawili ni wazawa

Kocha huyo Mcongomani amesema wiki ijayo baada ya mchezo kati ya Yanga dhidi ya Azam Fc anatarajiwa kuondoka kuelekea DR Congo kujiunga na timu ya Taifa kwa ajili ya kambi nchini Hispania

"Wiki ijayo naenda Congo kujiunga na timu ya Taifa, kabla sijaenda nitatangaza wachezaji niliowasajili na wengine ambao tumewaacha," alisema

"Msimu ujao tutakuwa na timu nzuri, itakayoweza kutupatia ubingwa na nafasi ya kushiriki michuano ya CAF"

Post a Comment

0 Comments