


KIPA wa timu ya Ndanda FC, Diel Makonga, amesema malengo yake katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao ni kuchezea timu mojawapo ya Kariakoo, Dar es Salaam, huku akisema tayari ameanza mazungumzo na Yanga.
Katika msimu uliomalizika kipa huyo alifanya mazoezi na Simba kwa muda wa wiki mbili hadi kufikia hatua ya kutaka kusajiliwa lakini ikashindikana kutokana na ujio wa Deogratius Munishi ‘Dida’.
Makonga alilimbia BINGWA jana kuwa, mkataba wake na Ndanda umeisha msimu uliomalizika na tayari kuna kigogo mmoja wa Yanga amemfuata kuzungumza naye.
Alisema kama atapewa ofa nzuri hatasita kwa sababu Yanga ni miongoni mwa timu zinazomvutia na anaamini uwezo wa kucheza kikosi cha kwanza anao.
“Mimi nina uwezo wa kucheza timu yoyote kubwa, unakumbuka Simba walitaka kunisajili katika msimu uliomalizika lakini dili likashindikana dakika za mwisho nikarudi Ndanda.
“Kuna kiongozi mmoja wa Yanga ameniambia nipo katika orodha ya makipa wanaowahitaji, hivyo nasubiria dili hilo kama litafanikiwa nitafurahi sana,” alieleza Makonga.



0 Comments