Kiungo wa Singida United Kenny Ally ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwaniwa na Yanga kwa ajili ya msimu ujao
Kenny anaweza kutua Yanga akiwa mchezaji huru kwani mkataba wake na Singida United unamalizika mwishoni mwa msimu huu
Uongozi wa Singida United umesema hauna pingamizi kwa kiungo huyo kama atapenda kujiunga na Yanga kwa kuwa maamuzi ni yake, mkataba wake uko ukingoni
"Kenny atakuwa huru kujiunga na timu yeyote baada ya ligi kumalizika, hivyo kama Yanga wanamuhitaji wazungumze nae," amesema Cales Katemana ambaye ni msemaji wa Singida United
Yanga imedhamiria kuunda kikosi cha ushindani kwa ajili ya msimu ujao
Tayari michakato ya usajili imeanza kimyakimya
0 Comments