Windows

KCCA mabingwa Uganda

Picha

TIMU ya KCCA mwishoni mwa wiki ilitangazwa kuwa bingwa wa Ligi Kuu ya StarTimes ya Uganda kwa mara ya 13, huku taji hilo likiwa ni la tano ndani ya misimu saba.

Taji hilo linaifanya KCCA kubakisha mataji matatu tu kabla ya kufikia rekodi ya Sports Club Villa, ambayo imetwaa ubingwa huo mara 16. Meneja wa KCCA, Mike Mutebi sasa anaamini kuwa klabu hiyo imeweka msingi imara, ambao unaweza kuwasaidia kutawala soka la Uganda kwa miaka kadhaa ijayo.

“Bado ni vijana wadogo na wengi wao wamehitimu kutoka katika timu yetu ya vijana, hivyo wana uwezo wa kutawala ligi na kushinda mataji ya ndani na nje ya nchi. Hivyo suala la uzoefu sasa halina nafasi tena,” alisema Mutebi ambaye binafsi anasherehekea taji la tatu katika misimu minne. “Wamesheheni wachezaji wenye uzoefu zaidi katika kipindi chao. Hivyo tuna kikosi ambacho kinaweza kutawala.

Tunataka kuwa na kikosi kipana, ambacho kitaundwa kutoka katika katika kikosi chetu cha vijana. Mfani msimu huu tumeweza kuwa na wachezaji 13 katika kipindi cha miaka minne na wengi wao wanapata nafasi ya kucheza,”aliongeza. Wawili kati ya vijana hao ni Allan Okello na Herbert Achai, ambao wamo katika orodha ya wapachika mabao siku ya mwisho wakati KCCA ilipoifunga Maroons kwa mabao 6-1 kwenye Uwanja wa StarTimes.

Bao la Achai lilivutia zaidi baada ya kuwapiga chenga mabeki wawili kabla hajaujaza wavuni mpira likiwa bao la mwisho alilofunga katika dakika ya 57 ya mchezo huo. Pia walikuwemo wachezaji wenye uzoefu mkubwa siku hiyo kama Allan Kyambadde, ambaye alifunga bao kabla ya lile la Achai. Pia kulikuwepo mabao kadhaa ya vichwa yaliyofungwa na Patrick Kaddu ambayo yamemwezesha kufikisha magoli 14 msimu huu pamoja na yale yaliyofungwa na Muzamir Mutyaba na Okello.

Post a Comment

0 Comments