

Katibu Mkuu wa Baraza la soka Afrika Mashariki (CECAFA) Nicholas Musonye amesema michuano ya kombe la Kagame mwaka huu itafanyika nchini Rwanda ikitarajiwa kuanza Julai 07 mpaka Julai 21
Simba watashiriki michuano hiyo wakiwa mabingwa wa Tanzania Bara wakati Azam Fc watshiriki wakiwa mabingwa watetezi
Miongoni mwa timu zilizoalikwa kushiriki michuano hiyo mwaka huu ni ZESCO United ya Zambia, AS Vita Club na DC Motema Pembe zote kutoka DR Congo
Musonye amesema timu hizo zimethibitisha kuwa zitashiriki
"Timu hizi ni kati ya klabu bora hapa barani Afrika na uwepo wao katika mashindano yetu utazisaidia kuzipa maandalizi mazuri klabu zetu ambazo mwakani zinashiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” amesema Musonye.
Simba, Azam FC, Gor Mahia ya Kenya na mabingwa wapya wa Ligi Kuu Rwanda, Rayon Sports ni baadhi ya timu zinazotarajiwa kushiriki katika mashindano ya mwaka huu ambayo bingwa wake atapata zawadi ya Dola za Marekani 30,000 wakati mshindi wa pili atajinyakulia Dola za Marekani 20,000 na timu itakayomaliza katika nafasi ya tatu itapata Dola za Marekani 10,000.
Kwa habari zaidi Download App ya Mwana Msimbazi kutoka Play Store. Bonyeza picha hapa chini



0 Comments