Windows

Kanye anapiga mkwanja kama WOTE!

  AGOSTI, 2015 wakati anazindua msimu wa pili wa mavazi yake ya Yeezy, staa wa Muziki wa R&B, Chris Brown alitumia ukurasa wake wa Instagram kuponda kinomanoma kuwa mavazi hayo yaliwahi kutumiwa katika Filamu ya The Hunger Game na kwamba ni ya watu maskini.

 

Maneno hayo yalikolezwa zaidi na mama wa kambo wa mke wa Kanye West, Kim Kardashian, Caitlyn pamoja na Rapa Jay Z ambaye alisema yanamuogopesha.

Pia katika uzinduzi mwingine wa mavazi hayo uliowahi kufanyika jijini London, Uingereza, Kanye alishambuliwa kuwa ni ya gharama wakati huku yakiwa yametengenezwa kama ya mtoto mdogo.

 

Ishu hiyo ilishambuliwa zaidi na Mwandishi wa Gazeti la NY Times, kuwa nguo hizo hazieleweki ni bora Kanye akabaki tu kwenye sanaa ya Hip Hop akaachana na mambo ya fasheni.

Hata hivyo, Kanye aliwajibu kwa jazba na kusema kwamba walikuwa hawamuelewi na pia hawaielewi fasheni na mapinduzi anayojaribu kuyaleta kwenye soko la mitindo, lakini ipo siku watamuelewa.

Alisema ni kitu ambacho anapenda kufanya tangu akiwa kijana na anajua kwamba yeye ni mkali kwenye ubunifu.

Licha ya kujitetea huko, Kanye amekuwa akiandamwa kila kona ya dunia hususan kwenye mitandao ya kijamii ambapo kila akitupia picha akiwa na mavazi hayo, huambulia za ‘uso’ na wengine wakimuona kama kichaa wakati nyuma ya pazia anapiga mkwanja kama wote kupitia mavazi hayo katika maduka mbalimbali aliyofungua sehemu mbalimbali duniani.

 

BEI ZAKE SASA

Katika mavazi hayo ya Yeezy, mengi yamebuniwa kwa kuchanwachanwa ambapo kama yakivaliwa Kibongobongo, basi utaonekana kama siyo muokota makopo, basi kichaa anayeishi kwa kula vyakula vya majalalani.

Kuna soksi anazoziita Bouclette ambazo kwa pea tatu anauza kiasi cha dola za Kimarekani 225 (zaidi ya shilingi 500,000 za Kibongo.)

Kuna masweta ya kutoboka na kuchanikachanika anayoyaita Free Hoover yanayopatikana kwa dola 700 (zaidi ya shilingi milioni 1.6).

Makoti ya kutobokatoboka yanayojulikana kama Bomber kwa dola 650 (zaidi ya shilingi milioni 1.4)

Suruali aina ya Calabasas dola 123 (zaidi ya shilingi 280,000). Jinzi dola 325 (zaidi ya shilingi 740,000) pamoja na makoti ya kijeshi yajulikanayo kama Camouflage Parka yanayopatikana kwa dola 1,700 (zaidi ya shilingi milioni 3.6).

KWENYE VIDEO

Licha ya kupondwa huko, leo hii mavazi hayo yanayojulikana kama Yeezy yameteka vijana na Kanye amekuwa akiyavaa nyumbani na hata watoto wake hutumia kuwavalisha.

Ameshaonekana na aina mojawapo ya mavazi hayo katika video ya wimbo wake wa I Love It aliomshirikisha Lil Pump ambayo yanamuonesha kama mfano wa boksi huku akiwa amevalia suruali lililomzidi pamoja na sendozi spesho ambazo nazo zimezidi miguu.

Katika video nyingine ya Figure It Out ya French Montana akiwashirikisha Nas na Kanye West, mavazi hayo yametumiwa kwa kiasi kikubwa.

KANISANI

Katika mavazi hayo pia aina nyingine ya Yeezy hutumia kwa wanakwaya wake katika kanisa lake la Kanye West Sunday Services ambalo hutoa ibada katika milima ya Coachella iliyopo California nchini Marekani kila siku ya Jumapili.

 

MKEWE HAVAI

Tangu Kanye azindue mavazi hayo, mkewe ambaye pia ni mwanamitindo na mtangazaji amekuwa akiyakwepa.

Hajawahi kuyavaa hadharani ikiwemo katika kipindi chao cha familia cha Keeping Up With The Kardashians ambacho wapo wadogo zake, Khloe, Kylie, Kourtney pamoja na mama yao, Kris Jenner.

The post Kanye anapiga mkwanja kama WOTE! appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments