


KLABU ya Simba yenye makao yake katika Mtaa wa msimbazi jijini Dar es salaam, leo Jumanne, Mei 28, 2019 imekabidhiwa rasmi kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa mwaka 2018/2019 baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.

Simba wamemaliza Ligi wakiongoza kwa pointi 93 mbele ya Yanga wenye pointi 86 na nafasi ya tatu ikishikwa na Azam wny pointi 78.

Mabingwa hao wa Soka Tanzania Bara wakishangilia Kombe la Ubingwa baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro

Stand United imeungana na African Lyon kushuka daraja, baada ya kufungwa 2-0 na JKT Tanzania.

Mwadui FC na Kagera Sugar zitacheza ‘Playoffs’ na Pamba FC pamoja na Geita FC kuwania nafasi ya kurejea ligi kuu.

Dakika 90 zimemalizika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Azam FC wanalipa kisasi. Yanga SC 0-2 Azam FC

MATOKEO
Yanga SC 0-2 Azam FC.
Coastal Union 0-0 Singida.
Ndanda 1-3 Mwadui.
JKT TZ 2-0 Stand United.
Ruvu Shooting 1-0 Alliance FC.
Mbeya City 0-0 Biashara.
Mbao FC 1-1 Kagera Sugar.
Tanzania Prisons 3-1 Lipuli FC.
African Lyon 0-2 KMC FC


PICHA NA MUSA MATEJA | GPL
The post KANGI LUGOLA AWAKABIDHI UBINGWA SIMBA SC – PICHAZ appeared first on Global Publishers.



0 Comments