Windows

Kamusoko awahi Zimbabwe kujiunga na timu ya Taifa



Kiungo wa Yanga Thabani Kamusoko ni miongoni mwa wachezaji 34 walioitwa kuunda kikosi cha awali cha timu ya Taifa ya Zimbabwe kitakachoshiriki fainali za AFCN 2019 zitakazofanyika nchini Misri kuanzia Juni 21 2019

Kamusoko tayari amejiunga na timu hiyo itakayoshiriki michuano ya COSAFA kabla ya baadhi ya wachezaji kuchujwa kwa ajili ya michuano ya AFCON

Kiungo wa Azam Fc Tafadzwa Kutinyu nae ameitwa kwenye kikosi cha timu hiyo, huku Donald Ngoma mshambuliaji wa Azam akishindwa kupata nafasi

Kamusoko amesema michuano hiyo ni fursa kwake, itamuimarisha zaidi na kumfanya arejee akiwa imara msimu ujao

Hatma ya kiungo huyo kuendelea kubaki Yanga itafahamika wiki ijayo

Post a Comment

0 Comments