SIKU chache baada ya kufanikiwa kuvunja mkataba na Yanga, aliyekuwa kipa namba moja wa timu hiyo, Beno Kakolanya amewaomba radhi wapenzi na mashabiki wa timu hiyo.
Ikimbukwe kuwa Kakolanya alifi kia hatua hiyo ya kuomba aachwe na Yanga ili akatafute maisha sehemu nyingine baada ya kocha mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera kugoma kufanya kazi naye kwa madai ya kuwa na utovu wa nidhamu, hata hivyo inadaiwa kuwa yupo karibuni kusaini Simba.
Akizungumza na Championi Jumatano, Kakolanya amewataka wapenzi na mashabiki wa Yanga wamsamehe kwa yote yaliyotokea kwani hakuwa na njia nyingine ya kufanya ili kuhakikisha analinda kipaji chake.
“Ni kweli kabisa hivi sasa mimi ni mchezaji huru na sina tena mkataba na Yanga kwani tayari umeshavunjwa na nishapewa barua inayoonyesha kuwa mimi ni mchezaji huru sasa.
“Hata hivyo, nimekuwa nikipokea simu mbalimbali kutoka kwa mashabiki wa Yanga wakinilaumu kuwa kuondoka kwangu ndiyo kumesababisha timu iwe hapo ilipo, ila naomba wajue kuwa siyo mimi niliyetaka niondoke.
“Lakini niwaombe tu msamaha kwa yote yaliyotokea kwani haya ni maisha tu, kwa hiyo haitapendeza kama kutakuwa na hali ya chuki dhidi yangu kutokana na hiki kilichotokea nafi kiri muda mchache mtafahamu nakwenda wapi,” alisema Kakolanya ambaye awali alikuwa kipa namba moja wa timu hiyo.
Sweetbert Lukonge, Dar es Salaam
The post Kakolanya Aomba Radhi Yanga SC appeared first on Global Publishers.
0 Comments