Mashabiki wa Msimbazi wana mzuka kama wote kutokana na chama lao kutavuna viporo vyao kwa kwenda mbele, lakini kumbe Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems akipiga hesabu za kubeba taji la Ligi Kuu Mapema akiwa kazi kina Meddie Kagere.
Kocha huyo ambaye anatarajiwa kusainishwa mkataba mpya wa mwaka mmoja, amesema kama nyota wake akiwamo Kagere, Emmanuel Okwi, John Bocco na Clatous Chama watafunga mabao mengi kuipa timu ushindi watalitetea taji lao mapema zaidi.
Aussems alisema wamekuwa wakitengeneza nafasi nyingi katika kila mchezo, lakini bado hawapati mabao mengi, hivyo anataka vijana wake waongeze moto ili wamalize kazi mapema.
"Siwezi kueleza idadi ya mabao ninayotaka ila napenda waongeze kasi yao, kwani wakifanya hivyo watarahisishia timu kupata pointi tatu, lakini halitakuwa jambo rahisi kwao kwa vile timu tunazocheza nao ni ngumu na zinakamia mno," alisema.
Simba ambayo jana ilikuwa Jijini Mbeya kuvaana na Prisons, inatarajiwa kuwa wenyeji wa Coastal Union katika mechi itakayopigwa Jumatano hii kwenye Uwanja wa Uhuru.
Aussems alisema ukaribu wa ratiba ni moja ya kikwazo cha kufanya vizuri lakini anajaribu kuwabadilisha wachezaji kila mechi ili wapate mapumziko na kuweza kuipa timu matokeo mazuri yatakayowafanya watetee taji kwa mara ya pili msimu huu.
Simba ipo nafasi ya pili nyuma ya Yanga inayoongoza na alama zao 77 baada ya mechi 34, huku Msimbazi wakicheza 29 wakifuatiwa na Azam iliyopo nafasi ya tatu na pointi 66 baada ya mechi 33.

0 Comments