Windows


Huko Jangwani michakato ya usajili ni kama yote. Mchana na usiku wachezaji wanapishana 'kusinya' mikataba kuwatumikia mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga

Hata hivyo bado uongozi wa Yanga haujatoa taarifa rasmi, ikielezwa kuwa wameamua kukamilisha sehemu kubwa ya usajili kabla ya kwenda hewani kuweka hadharani kila kitu

Ukipita Jangwani, yalipo Makao Mkuu ya Yanga, muda wote mashabiki wamefurika wakishuhudia vifaa vinaingia na kutoka!

"Eti wanasemaje huko kuhusu usajili?. Tuwe na subra, tumuache Mwalimu asuke kikosi na muda ukifika kila kitu kitakuwa wazi," imesema taarifa fupi iliyotolewa na Yanga

Uongozi wa Yanga pamoja na benchi la ufundi chini ya kocha Mwinyi Zahera wamedhamiria kuunda 'kikosi cha mauaji' kitakachokuwa na uhakika wa kurudisha ubingwa Jangwani baada ya kuukosa kwa misimu miwili

Kwa yanayoendelea huko Jangwani, hakika kuna watu wanapaswa kujiandaa kisaikolojia

Mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye yuko kwenye Kamati ya usajili amesema shughuli ndio kwanza inaanza, usajili wa sasa ni rasha-rasha, bado kuna 'mashine' kali hazijawasili

Aidha baadhi ya wachezaji bado hawajamaliza mikataba na timu zao hivyo kuepuka kuingia matatani, uongozi wa Yanga hauwezi kuwatangaza sasa mpaka mikataba yao ya timu wanazozichezea sasa imalizike


Post a Comment

0 Comments