KWA sasa Ubingwa wa Ligi Kuu kwa timu mbili za Simba na Yanga ni hesabu tu zinachezwa ili kuona ni namna gani bingwa atapatikana msimu huu.
Azam wao tayari hesabu zimewakataa baada Yanga kuwafunga Uwanja wa Uhuru pamoja na sare ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Kambarage jana, hivyo kwa sasa vita imebaki kwa Yanga ambao wapo kileleni kwa pointi 80 baada ya kucheza michezo 34 wamebakiza mechi nne.
Simba wamecheza mechi 30 wana pointi 78 wamebakiza michezo 8 kukamilisha mzunguko wa pili.Azam nafasi ya tatu wamecheza michezo 34 wana pointi 67 wamebakiwa na michezo minne.
Mechi nane zimeshikilia Ubingwa wa Simba na nne zimeshikilia kwa Yanga endapo atashinda kombe linarejea Msimbazi kimahesabu mechi 8 ambazo amebakiwa nazo akishinda zote atafikisha jumla ya pointi 102 huku Yanga akishinda nne zote atafikisha pointi 92.
Simba akishinda mechi tano mfululizo kwa sasa atafikisha jumla ya pointi 93 ambazo hazitafikiwa na Yanga na kumfanya awe bingwa tena akizubaa anapigwa bao na Zahera ambaye amesema hapotezi hata moja ni hizi hapa ngumu kwa Simba:-
Mei 8, Simba v Coastal Union, Uwanja wa Uhuru, Dar. mchezo huu Simba kama atashinda atamshusha Yanga kileleni kwa mara ya kwanza kwa kuwa atafikisha jumla ya pointi 81
Mei 10, Simba v Kagera Sugar, Uwanja wa Uhuru.
Mei 13, Simba v Azam FC, Uwanja wa Taifa.
Mei 16, Simba v Mtibwa Sugar, Uwanja wa Taifa.
Mei 19, Simba v Ndanda, Uwanja wa Taifa.
Mei 22, Singida United v Simba, Uwanja wa Taifa.
Mei 25, Simba v Biashara United, Uwanja wa Taifa.
Mei 28, Mtibwa v Simba, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Kwa upande wa Yanga, Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera amesema kuwa anaamini Simba itateleza mahali kisha yeye atajipigia hawa jamaa kisha abebe kombe lake kama ifuatavyo:-
Mei 9 Biashara United v Yanga, Karume.
Mei 14 Ruvu Shooting v Yanga Uwanja wa Mabatini.
Mei 22 Yanga v Mbeya City Uwanja wa Taifa.
Mei 28 Yanga v Azam FC uwanja wa Taifa.
Hivyo suala la bingwa mpya msimu huu ni jambo la kusubiri kwanza ligi bado mbichi.
0 Comments