Mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji Eden Hazard bado ameendelea kulikwepa swali kuhusiana na hatma yake ya ndani ya Chelsea, Hazard amekuwa akihusishwa mara nyingi na mpango wa kwenda kujiunga na Real Madrid ya Hispania mwisho wa msimu wa 2018/2019 lakini nyota huyo amekuwa akijibu linalotoa majibu ya nusu kwa nusu uwezekano wa suala hilo kuwepo.
Hazard baada ya kumalizika kwa mchezo wa nusu fainali ya Europa League na kumalizika kwa Chelsea kupata ushindi wa mikwaju ya penati 4-3 (1-1) dhidi ya Frankfurt, Hazard aliulizwa swali kuwa mchezo wa fainali ya Europa League dhidi ya Arsenal May 29 katika uwanja wa Olympic mjini Baku, ndio utakuwa mchezo wake wa mwisho akiwa na Chelsea au?
“Sifikiri kuhusiana na hii kuwa ni mechi yangu ya mwisho, nafikiria kuhusiana na kushinda taji kwa ajili ya club hii na kikosi hiki, kama ni mechi yangu ya mwisho nitajitahidi kufanya kila kitu kwa ajili ya hii club ili ishinde Kombe ila kichwani kwangu sijui kama hii ndio game yangu ya mwisho Chelsea”>>>Eden Hazard
0 Comments