Windows

Bajeti ya usajili Simba ni mara mbili ya msimu uliopita



Jana Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya timu ya Simba Sc Mohammed Dewji 'Mo' aliwatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuwa watafanya usajili wa maana zaidi ya msimu uliopita

Tofauti na msimu uliopita, msimu huu Simba imekuwa wakiwaacha watani zao Yanga wakitawala vyombo vya habari kwa kufanya usajili 'kwa fujo'

Akizungumza jana kwenye hafla ya Mo Simba Awards iliyofanyika Hotel ya Kilimanjaro jijini Dar es salaam, Mo alisema Simba haijaanza michakato ya usajili lakini watakapoanza mashabiki na wanachama wa timu hiyo watafurahi

"Ndio kwanza tumepokea taarifa ya benchi la ufundi kuhusu maboresho ya kikosi chetu," alisema Mo

"Sio kwa wachezaji wapya tu, hata wachezaji tunaoendelea nao ambao mikataba yao imemalizika bado hatujawapa mikataba mipya"

"Tunakusudia kulianza zoezi hilo wiki ijayo baada ya kikao cha Bodi ya Wakurugenzi"

"Lakini nawahakikishia Wanamsimbazi kuwa wachezaji wote waliomaliza mikataba tutawabakisha kwa gharama yoyote"

"Lakini pia tumetenga bajeti ya usajili ambayo ni mara mbili ya ile tuliyotumia msimu uliopita, hivyo hakuna wasiwasi fedha tunazo za kutosha"cut

Msimu uliopita Simba ilitumia Tsh Bilioni 1.3 na kwa kauli hiyo ya Mo, msimu huu itatumia zaidi ya Bil 2.6 kwa ajili ya usajili

Aidha inaelezwa Simba haina haraka ya kufanya usajili kwa kuwa inahitaji wachezaji ambao wana uwezo wa hali ya juu

Itatumia michuano ya AFCON 2019 inayoanza mwezi ujao nchini Misri kufanya 'scouting' ya wachezaji wa kigeni ambao watasajiliwa na timu hiyo

Post a Comment

0 Comments