

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amefunga bao la pili, timu yake KRC Genk ikiibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Royal Antwerp FC kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
Samatta alifunga bao lake dakika ya 55, baada ya kiungo wa kimataifa wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy kufunga la kwanza kwa penalti dakika ya 25, kabla ya mshambuliaji Mjapan, Junya Ito kufunga la tatu dakika ya 57 na kiungo Mbelgiji, Bryan Heynen Heynen kufunga la nne kwa penalti pia dakika ya 90
Ushindi huo unaifanya Genk ifikishe pointi 50 katika hatua ya pili ya Ligi ya Ubelgiji, maarufu kama Chama Championship Round na kuendelea kuongoza, ikifuatiwa na Club Brugge yenye pointi 41.
Kwa Samatta jana amefunga bao lake la 23 la msimu na la tatu katika Championship Round akiwa anaendelea kuongoza kwenye mbio za ufungaji bora.
Kwa ushindi huu Genk imebakiza mechi tatu ligi hiyo iweze kumalizika huku wakihitaji pointi 4 tu ili watawezwe kuwa mabingwa wapya wa msimu huu endapo Club Bruge akipoteza mechi moja kati ya nne alizobakiza Samatta atabeba taji hilo
Kikosi cha KRC Genk jana kilikuwa; Vukovic, Maehle, Aidoo, Dewaest/Seigers dk89, Uronen, Berge, Heynen, Malinovskyi/Wouters dk67, Ito, Trossard na Samatta/Gano dk84.
Royal Antwerp FC; Bolat, Juklerod, Rodrigues/Bolingi dk77, Baby/Owusu dk63, Arslanagic, Simao/Refaelov dk68, Govea, Van Damme, Haroun, Yatabare na Mbokani.







0 Comments