Windows

Azam yabanwa Shinyanga, KMC yaipiga Mwadui

Test



Azam FC wamelazimishwa sare ya bao 1-1 na Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Mshambuliaji Danny Lyanga ndiye aliyeanza kupachika bao, akiitanguliza Azam FC dakika ya 17, kabla ya wenyeji Stand United kutulia na kuonesha kandanda safi lililowafanya kupata bao la kusawazisha dakika ya 70 kupitia kwa Afidhi Mussa.
Kwa matokeo hayo kila timu imechukua pointi moja ambapo Azam wamefikisha pointi 67 na kuendelea kukaa nafasi ya tatu huku Stand United wakitoka nafasi ya 16 hadi ya 13 baada ya kufikisha pointi 39.
Katika mchezo mwingine uliopigwa leo, KMC imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mwadui FC mchezo ukipigwa kwenye Dimba la Uhuru Dar es Salaam.
Mabao ya KMC yamefungwa na Yusuph Ndikumana dakika ya 50 na Masoudy Abdallah dakika ya 84. Sasa KMC imefikisha pointi 45 katika nafasi ya 6 huku Mwadui wakishuka hadi nafasi ya 19 wakiwa na pointi zao 37.

Post a Comment

0 Comments