Kocha wa Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa lazima walipe kisasi kwenye Uwanja wa nyumbani baada ya kupoteza mchezo wao mbele ya Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Manungu
Cheche amesema kuwa wanakumbuka walifungwa mabao 2-0 ugenini hivyo nao wamejipanga kupata pointi tatu uwanja wa nyumbani.
"Tulipoteza mchezo wa kwanza, hivyo benchi la ufundi limetulia na kufanyia kazi makosa ya mchezo uliopita, mipango ipo sawa tunaimani tutalipa kisasi mchezo wetu utakoachezwa uwanja wa nyumbani.
"Kupoteza kwetu mchezo wa kwanza kulikuwa na sababu za kiufundi hivyo tumepata majibu ya kiufundi tutazijibu kiufundi," amesema Cheche.
Kikosi cha Azam FC, kitaikaribisha Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa ligi, uwanja wa Azam Complex Mei 22 mwaka huu saa 2:00 usiku.
0 Comments