UONGOZI wa Klabu ya Azam FC umefanya kweli baada ya kumwongezea mkataba mpya wa miaka miwili beki wao Mghana Yakub Mohammed aliyekuwa anawindwa na Simba.
Inadaiwa Simba walikuwa wanapiga hesabu kali kuhakikisha wanamsajili mchezaji Yakub ambaye ameonyesha kiwango kizuri katika nafasi hiyo ya ulinzi lakini kilichomkwamisha ni makubaliano ya kimaslahi.
Leo Alhamisi mchana uongozi wa Azam FC walifanya kweli na kumwongezea mkataba wa kipindi hicho na hivyo kukata matumaini ya vigogo wa Simba kumnasa beki huyo.
Yakub amekuwa katika kiwango kizuri ndani ya kikosi cha Azam FC tangu alipojiunga mwaka 2017.
Mkataba wa awali wa Yakub ulikuwa unamalizika Desemba mwaka huu lakini kutokana na purukushani hizo, Azam wakahakikisha anabaki kwao kwa ajili ya msimu ujao.

0 Comments