KIKOSI cha Stand United chenye maskani yake mkoani Shinyanga kimepoteza kabisa matumaini ya Azam FC kutwaa kombe la Ligi Kuu msimu huu.
Vita ya ubingwa kwa sasa ni kati ya Yanga ambao ni vinara wakiwa napointi 80 na Simba ambao wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 78.
Bao la kipindi cha kwanza dakika ya 17 kupitia kwa Dany Lyanga kwa pasi ya Mudathir Yahya halikufua dafu kwani kipindi cha pili dakika ya 70 Stand United walisawazisha kupitia kwa Alfadhil Mussa.
Ushindi huo Azam FC wanagawana pointi moja na kubaki nafasi ya tatu wakiwa na pointi 67 baada ya kucheza michezo 34 na wana michezo minne ili kukamilisha mzunguko wa pili na kuhitimisha msimu huu kwenye ligi kuu.
Kama Azam wakishinda michezo yote minne watajikusanyia pointi 12 ambazo zitawafanya wawe na jumla ya pointi 79 ambazo tayari zimeshafikiwa na vinara wa ligi Yanga ambao wamecheza michezo 34 na wana pointi 80 hivyo Stand United wametibua malengo ya Azam Fc msimu huu.
Mchezo wao unaofuata ni dhidi ya KMC ambao wapo nafasi ya 6 kwenye msimamo wakiwa na pointi zao 45 utakaochezwa uwanja wa Chamazi kesho.
0 Comments