BAADA ya Simba juzi kutangaza ubingwa rasmi, kocha wake Patrick Aussems ametuma ujumbe wenye vijembe kwa watani zao Yanga juu ya taji hilo.
Aussems ametoa ujumbe huo kwa watani zao hao kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter juzi kabla ya mechi ya Yanga na Mbeya City.
“Kwenye nchi nyingine, mshindani wetu akiwa na pointi 83 na amebakiza mechi mbili anakuwa bingwa, lakini Tanzania kuna Simba, shukrani wachezaji kwa msimu mzuri kwenye historia ya klabu na shukrani kwa mashabiki kwa sapoti yenu, This is Simba,” aliandika kocha huyo.
Kabla Yanga hajacheza na Mbeya City alikuwa na pointi 83 na mechi mbili mkononi, hivyo hakuna shaka kwamba kijembe hicho kilienda kwa Yanga ambayo kocha wake Mwinyi Zahera mara kadhaa amekuwa akilalamika akidai Simba haikuwa na uwezo wa kutwaa ubingwa bali inabebwa.
Simba ilitetea taji la Ligi Kuu mwishoni mwa wiki iliyopita kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida United na kufikisha pointi 91 ambazo hziwezi kufikiwa na timu yoyote. Kwani Yanga ikishinda mechi yake ya mwisho itakuwa na pointi 89. Hilo linakuwa taji la 20 kwa Simba huku wakiwa na kibarua kigumu cha kuwafukuzia wapinzani wao Yanga waliotwaa taji hilo mara 27.

0 Comments