Windows

Ajibu atatesa TP Mazembe - Zahera

Picha

KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema Ibrahim Ajibu anaweza kufanya makubwa kwenye klabu ya TP Mazembe ya Congo iwapo atakwenda kujituma. 

Ajibu mkataba wake unaelekea ukingoni na anatarajiwa kujiunga na Mazembe baada ya klabu hiyo kutuma barua Yanga kuomba uthibitisho wa mchezaji huyo kumaliza mkataba wake.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari juzi kuhusu mchezaji huyo, Zahera alisema Ajibu ni mchezaji mzuri mwenye akili ya mpira hivyo, akienda Mazembe atapandisha kiwango chake na 

kuwa bora zaidi. “Ajibu ni mchezaji mzuri na anaweza kufanya vizuri iwapo atakwenda kujituma ila anatakiwa ajue TP Mazembe ni timu yenye nguvu sana akienda akikaa hatacheza,” alisema.

Zahera alisema mchezaji huyo akienda Mazembe hatokuwa nyota peke yake kwa sababu wapo wengi, kwa hiyo huenda akatumia nafasi ya kuboresha kiwango chake ili kuwa sawa na wengine atakaowakuta. Mchezaji huyo wa zamani wa Simba alijiunga na Yanga msimu wa mwaka juzi kwa mkataba wa miaka miwili na huu ni msimu wake wa mwisho.

Kabla ya taarifa hizo za Mazembe, Ajibu alitajwa huenda akarejea Simba baada ya kudaiwa kusaini mkataba wa awali. Katika hatua nyingine, kocha huyo msaidizi wa timu ya taifa ya Congo alisema anatarajiwa kusafiri Ulaya Mei 28, mwaka huu usiku baada ya kumalizika kwa mechi ya mwisho dhidi ya Azam FC. Kabla ya kuondoka, alisema atahakikisha anaacha majina manane ya kusajiliwa ambapo kati ya hayo, sita wa kigeni na wawili wa soka la hapa nchini.

Post a Comment

0 Comments