

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kwa sasa Waamuzi wamekuwa wakiogopa kuwapa Simba penati pale zinapotokea Uwanjani.
Aussems ameeleza kuwa tangu wapewe pointi tatu walipocheza dhidi ya KMC imeonekana kama timu yake inatengenezewa mazingira ya kushinda.
Kauli ya Aussems imekuja kutokana na moja ya tukio la mchezaji Emmanuel Okwi kuchezewa rafu eneo la hatari mwa Mbeya City jana walipocheza mchezo wa Ligi Kuu, lakini Mwamuzi akapeta.
"Tangu tupewe penati mbili katika mchezo dhidi ya KMC inaonekana kuna maagizo yametolewa kuwa tusipewe penati tena.
"Marefa wanaogopa kutupa penati maana kuna penati halali ambazo hatupewi.
"Sijajua tatizo ni nini cha msingi tumeshinda tumepata pointi tatu ndiyo lilikuwa hitaji letu.
"Sasa tunajiandaa na mchezo ujao."




0 Comments