Windows

Ajibu awapeleka TP Mazembe kwa mama yake

 Mabosi wa TP Mazembe jioni hii watakutana na mama yake mzazi Ibrahimu Ajib kujadilia hatma ya mshambuliaji huyo aliyehaidiwa mshahara wa dola 5000 kwa mwezi akijiunga nao.

Pamoja na kuwepo kwa taarifa kuwa mabingwa hao wa Afrika mara tano, TP Mazembe wamefuta mpango wa kumsajili nyota huyo, lakini viongozi wa klabu hiyo wapo jijini Dar es Salaam kwa takribani wiki sasa kwa lengo la kumaliza usajili Ajibu.


Mmoja wa maofisa wa TP Mazembe amesema kocha wa TP Mazembe, Mihayo Kazembe na benchi lake la ufundi wanamtaka Ajibu na ndio maana wako Dar es Salaam hadi leo.


"Tangu tumefika hatujaonana na Ajibu isipokuwa ndugu yake tumeongea naye kwenye simu. Lengo ajiunge na TP Mazembe, lakini inavyoonekana kama hayuko tayari," alisema jamaa huyo.


"Tumeongea na kaka yake ametuhakikishia Ajibu hajasaini Simba, ametuambia tuonane na mama yake jioni hii na yeye atakuwepo, tunamsubiria.


"Kwa sasa alionekana tatizo linaonekana katika fedha pesa, yeye anataka nyingi zaidi ya ofa yetu TP Mazembe na wakati awali alikubali tena ilikuwa ndogo kabisa."

Post a Comment

0 Comments