

Kocha Mwinyi Zahera amesema uamuzi wa wachezaji kugomea mazoezi sababu ya kutolipwa mishahara yao kwa zaidi ya miezi minne KIMEMKERA kwa kuwa wachezaji hawakumshirikksha.
Wachezaji wa Yanga leo wamefika mazoezini leo asubuhi Polisi barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, lakini hawakufanya mazoezi wakishinikiza kulipwa mishahara yao.
Kocha huyo amefunguka kuwa amechukizwa na kitendo hichi akieleza wachezaji wake walifanya bila kutoa taarifa.
Aidha amesema kwa wale ambao hawatafika kwenye mazoezi ya kesho atawafukuza moja kwa moja wakakae makwao sababu hawana nia ya kuichezea Yanga.
Una maoni yoyote juu ya maamuzi ya Zahera?




0 Comments