Windows

ZAHERA AIPA ONYO TFF, AWANYANG'ANYA SIMBA UBINGWA MSIMU HUU


Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amewatahadharisha Shirikisho la Soka Tanzania kuwa makini na ratiba ya Ligi Kuu Bara msimu huu.

Zahera ameeleza kuwa iwapo TFF watakuwa makini na uendeshaji wa ratiba ya ligi ana uhakika wa Yanga kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Kocha huyo mwenye maneno mengi amefunguka kwa kueleza kuwa timu yake ina uhakika wa kutwaa kikombe msimu huu endapo atashinda mechi zake 10 zilizobaki msimu huu.

Mbali na kushinda amewaombea Simba kupoteza walau mechi 3 kati ya 10 zilizosalia kwao ili kuwapa mwanya wa kukirejesha kikombe hicho baada ya kuchukuliwa na watani zao msimu uliopita.

Wakati huo kikosi cha Yanga leo kinashuka dimbani kucheza dhidi ya Ndanda katika mchezo wa ligi utakaopigwa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.


Post a Comment

0 Comments