Windows

Tottenham yaufungua rasmi uwanja mpya kwa ushindi

Bao la mapema la Kevin De Bruyne lilisaidia kuirejesha Manchester City kileleni mwa ligi baada ya kupata ushindi wa 2 – 0 dhidi ya Cardiff City uwanjani Etihad.

City walihitaji ushindi ili kuwaondoa Liverpool kileleni. City waliutawala mchezo mzima huku Leroy Sane akiongeza bao la pili na kuhakikisha kuwa vijana hao wa Pep Guardiola wanabaki na pointi zote tatu.

Chelsea 3 – 0 Brighton

Callum Hudson-Odoi alianza katika kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza katika ligi wakati Chelsea ikipata ushindi mwepesi wa 3 – 0 dhidi ya Brighton. Matokeo hayo yameziongeza shinikizo mahasimu wao wanaowania nafasi ya nne Tottenham Hotspur na Arsenal.

Odoi alimuandalia pasi safi Olivier Giroud ambaye hakusita kucheka na wavu katika kipindi cha kwanza. Chelsea ilipata bao la pili kupitia Eden Hazard kabla ya Reuben Loftus-Cheek kufunga la tatu na la mwisho.

Spurs 2 – 0 Crsytal Palace

Majina yao yataandikwa katika madaftari ya kumbukumbu. Mabao ya kipindi cha pili ya Son Heung-min na Christian Eriksen yalitosha kuufungua rasmi uwanja mpya wa Tottenham Hotspur. Sasa wamesonga hadi nafasi ya tatu, pointi moja mbele ya Arsenal na Chelsea.


Post a Comment

0 Comments