

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars itacheza mchezo wa kirafiki wa Kimataifa na Timu ya Taifa ya Misri Juni 13,2019 Bourg Al Arab, Misri kujiandaa na Fainali za Afrika (Afcon2019).
Stars imefuzu kushiriki michuano ya Afcon baada ya kushinda mchezo wa mwisho mbele ya Uganda kwa mabao 3-0 mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwenye makundi ya Afcon imepangwa kundi C ambalo lina timu kama Kenya, Algeria na Senegal ambao ndio wataanza kucheza nao kwenye mchezo wa kwanza nchini Misri.



0 Comments