UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa sasa kilichobaki kwa kila timu ni lazima ishinde mechi zake ili kubeba ubingwa na hilo likiwezekana watakaa juu kwa tofauti ya pointi 10 huku wapinzani wao Yanga wakiendelea kupeta.
Ofisa wa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa ubingwa wa ligi upo mikononi mwao hivyo wana uhakika wa kuutwaa tena msimu huu.
"Sisi ni mabingwa wa Taifa hili na ubingwa wa msimu huu upo milkononi mwetu, yaani kila mtu akishinda zake tutakaa juu kwa points kumi.
"Tukutane kesho pale Uwanja wa Uhuru kuzisaka tatu pointi tatu muhimu, slogan yetu kila mtu ashinde zake hesabu tutazikuta mwambani," amesema Manara.
Kama Simba atashinda mechi zake 11 zilizobaki itajikusanyia jumla ya pointi 33 na kufanya wawe na jumla ya pointi 102, Yanga kama watashinda mechi zote 5 zilizobaki itajikusanyia pointi 15 na kufanya ifikishe jumla ya pointi 92.
0 Comments