Windows

JKT TANZANIA YAPANIA KUISIMAMISHA SIMBA KESHO


KOCHA Mkuu wa JKT Tanzania, Abdallah Mohamed 'Bares' amesema kuwa kesho atapambana kupata matokeo mbele ya Simba kutokana na maandalizi aliyoyafanya kwa muda aliokuwa na kikosi.

Bares ambaye mchezo wake wa kwanza alishinda mbele ya Mbeya City, kesho atashusha muziki mzito kuimaliza Simba ambayo ipo kwenye kampeni ya kushinda mechi zake ili kutetea ubingwa.

"Tumejipanga kupata matokeo mbele ya Simba, tupo tayari na tuna imani ya kupata matokeo mbele ya kikosi cha Simba kesho.

"Nakitambua vema kikosi cha Simba pamoja na mbinu zake hivyo hawanipi shinda, nimewapa mbinu mpya na kali vijana wangu, hivyo sapoti ya mashabiki muhimu," amesema Bares.

Mchezo huo utachezwa kesho Uwanja wa Uhuru, majira ya saa 10:00 Jioni.


Post a Comment

0 Comments