Windows

REKODI YA BEKI JOHN TERRY YAVUNJWA BAADA YA KUPITA MISIMU SITA



TUZO ya mchezaji bora wa mwaka 2018-19 aliyoibeba jana beki wa Liverpool, Virgil Van Dijk imevunja rekodi iliyowekwa kwa muda wa misimu sita baada ya kubebwa kwa mara ya kwanza na beki wa Chesea John Terry msimu wa mwaka 2004-05.
Dijk alitwaa tuzo hiyo iliyokuwa mikononi mwa mchezaji mwenzake Mohamed Salah ambaye alitwaa msimu uliopita wa mwaka 2017-18.
Beki huyo mwenye miaka 27 aliwapoteza washindani wenzake ambao alikuwa akishindana nao ikiwa ni pamoja na Raheem Sterling, Bernardo Silva, Sergio Aguero, Sadio Mane na Eden Hazard.
Pia mshabuliaji wa kikosi cha timu ya wanawake ya  Arsenal Vivianne Miedema mwenye miaka 22 alitwaa tuzo ya mchezaji bora baada ya kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa akiwashinda  wenzake kama Steph Houghton, Nikita Parris, Keira Walsh, Erin Cuthbert na Ji So-yun.
Miedema amesaidia timu yake hiyo ya Arsenal kutwaa kombe hilo baada kupita misimu mitatu mara ya mwisho kutwaa ubingwa huo ilikuwa mwaka 2012.


Post a Comment

0 Comments