Windows

AUSSEMS: TUMERUDI DAR, KAZI BADO


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amefunguka kuwa wanarudi jijini Dar kujipanga zaidi baada ya kukusanya pointi tisa kwenye mechi zao nne za Kanda ya Ziwa.

Kikosi hicho kilirejea Dar jana Jumapili Kikitokea mkoani Mara ambapo kilikuwa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United na Kushinda 2-0.

Mechi nyingine Simba Walizocheza Kanda ya Ziwa na kushinda ni dhidi ya Alliance na KMC, huku wakifungwa na Kagera Sugar.

Aussems ameliambia Championi Jumatatu, kuwa wanarudi Dar kujipanga zaidi kwa ajili ya mechi zao zijazo za ligi ambazo wanataka kushinda ili kukaa juu ya msimamo wa ligi.

“Ni furaha kushinda mechi yetu ya mwisho Musoma na kupata pointi ambazo tulikuwa tunazitaka. Nimeridhika na utendaji wa kazi wa kikosi change katika mechi za Kanda ya Ziwa.

“Kwa sasa tumerudi Dar kuja kujipanga kwa ajili ya mechi zetu zijazo, lengo ni kushinda ili kukaa juu kwenye msimamo wa ligi,” alisema kocha huyo raia wa Ubelgiji.

Mechi inayofuata ya Simba ni kesho Jumanne dhidi ya JKT Tanzania katika Ligi Kuu Bara itakayochezwa jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments