MSANII wa Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, anayesumbua kwa sasa na ngoma yake ya 'Your Are The Best' amesema kuwa katika maisha yake anapenda kusaidia jamii kwa kila anachoweza bila kumbania mtu yoyote.
Dimpoz amesema kuwa binadamu wanapaswa watambue kuwa duniani ni mapito na kusaidiana ni jambo la kheri kwa kila anayefanya hivyo bila kuwa na sababu ya kuwa na roho mbaya.
"Imani yangu ni kwamba riziki ya mtu ipo popote hivyo sina ulazima wa kumbania mtu yoyote katika jambo lolote, naamini kwenye upendo na kujitoa," amesema Dimpoz.
0 Comments