KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa mchezo wa leo kwake sio mwepesi kutokana na kikosi anachokabiliana nacho cha Azam FC kuwa na mwenendo mzuri.
Zahera amesema kuwa hakuna tofauti kubwa kwa maandalizi ya kikosi chake ila amewatahadharisha wawe makini na mwenendo wao ambao haumridhishi hasa kwa kushindwa kuwa na nidhamu uwanjani.
"Kikubwa ambacho kimekuwa na ugumu kwetu na kinatusumbua ni maneno hivyo wachezaji wangu nimewaelekeza wacheze kwa nidhamu na kujituma kwenye mchezo wetu wa leo ili kupata matokeo.
"Kwa upande wa mbinu na mipango hiyo ipo sawa kutokana na maandalizi ambayo tumeyafanya kwa muda mrefu na kukaa na timu, hivyo mahabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti," amesema.
Yanga itakuwa ugenini leo kumenyana na Azam FC huku mchezo ukiwa ni mchezo wao wa kwanza msimu huu kukutana.
0 Comments