Windows

Mazembe yafungwa 1 – 0 ugenini dhidi ya Esperance

Klabu ya Esperance de Tunis imepata ushindi mwembamba ila muhimu dhidi ya TP Mazembe ya Congo wa 1-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa ligi ya mabingwa Afrika, mtanange uliochezwa uwanja wa Olympic Rades Jumamosi.

ES Tunis walifanikiwa kupata goli la nyumbani litakaloipa faida katika mchezo wa raundi ya pili utakaochezwa uwanja wa TP Mazembe, Stade TP Mazembe, Lubumbashi, Mei 4.

Timu zote zikiwa zimewai kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa, zilitengeneza nafasi kwa kila upande huku Taha Khenissi juhudi zake zikiishia mikononi mwa mlinda mlango wa Mazembe, lakini pia Meshack Elia alijaribu ingawa hakufanikiwa.

Mpaka kipenga cha mwamuzi kinapulizwa kuashiria kumalizika kwa kipindi cha kwanza Esperance Tunis 0-0 TP Mazembe, licha ya kosa kosa za hapa na pale kwa timu zote mbili.

Kipindi cha pili kilihitaji dakika sita pekee kupokea goli la kuongoza upande wa Esperance Tunis kupitia mpira wa krosi ulioenda moja kwa moja wa Youcef Belaili.

Juhudi za kurudisha goli za Mazembe ziligonga mwamba baada ya mlinzi wao Kabaso Chongo kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kunako dakika ya 20 ya mtanange huo.

Dakika 90 zinakamilika kwa Esperance De Tunis kushunda goli 1-0 ya TP Mazembe. Mchezo wa mkondo wa pili utafanyika Mei 4 Lubumbashi, huku Mazembe wakihitaji ushindi wa goli mbili au zaidi.

Vikosi vya timu zote mbili :-

Esperance: Ben Cherifa, Meskini, Dhaouadi, Chemmam (Bguir 75’), Ben Mohamed, Kom, Coulibaly, Elhouni (Badri 32’), Chaalali, Belaili, Khenissi (Jouini 70’)

Mazembe: Gbohouo, Mpeko, Zatu, Chongo, Zola, Miche, Sinkala, Koffi, Muleka, Mputu (Malango 61’), Elia


Post a Comment

0 Comments