Kocha mkuu wa Borussia Moenchengladbach Dieter Hecking atajiuzulu mwishoni mwa msimu huu. Hayo yamethibitishwa na klabu hiyo ya ligi kuu ya kandanda Ujeurmani – Bundesliga.
“hatutarefusha ushirikiano wetu na Dieter Hecking baada ya kukamilika msimu huu na tutaanza msimu mpya wa kandanda na kocha mkuu mpya.
Hecking mwenye umri wa miaka 54, amekuwa usukani katika klabu ya Galdbach tangu Desemba 2016, na akaiongoza kumaliza katika nafasi ya tisa katika misimu yake miwili ya kwanza. Baada ya kuwa na mchezo mzuri sana mwanzoni mwa msimu huu, Gladbach kwa muda mrefu ilikuwa katika kundi la timu tatu za kwanza kwenye ligi, lakini mfululizo wa matokeo mabaya ya karibuni umewafanya kuanguka hadi nafasi ya tano.
Wameshinda mechi moja tu kati ya zao saba za mwisho, na mwishoni mwa wiki walibamizwa 3 – 1 mikononi mwa watani wao Fortuna Düsseldorf.
0 Comments