UONGOZI wa KMC umesema kuwa wamejipanga kiasi cha kutosha kuibuka na pointi tatu mbele ya Mbeya City uwanja wa Sokoine saa 10:00 jioni kama ambavyo walifanikiwa kubeba pointi tatu mchezo wao wa kwanza.
Ofisa Habari wa KMC, Anwari Binde amesema kuwa mbinu za kocha Kocha Mkuu, Ettiene Ndayiragije zimepenya vizuri kwa vijana wao ambao wanashuka leo uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao mbele ya Ndanda FC.
"Makosa ambayo yamepita tumeyafanyia kazi na sasa tupo tayari kwani kocha mkuu tayari amewapa mbinu vijana kinachosubiriwa ni dakika tisini tu kukamilika tusepe na pointi," amesema Binde.
KMCipo nafasi ya tano imecheza michezo 30 ikiwa na pointi 41 imeshinda mechi 9, sare 14 na kupoteza michezo 7 imefunga mabao 32 na kuruhusu kufungwa mabao 22 mchezo wa kwanza waliitungua Mbeya City bao 1-0 Uwanja wa Uhuru.
0 Comments