Windows

KISA UONGOZI WA MUDA YANGA, AKILIMALI AWA MBOGO TENA, ATOA TAMKO LA KUTISHA


Imeelezwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga Mzee Ibrahim Akilimali amendelea kusisitiza Baraza la wadhamini hawana mamlaka ya kuteua uongozi wa muda ndani ya klabu.

Akilimali amefunguka kwa kueleza kuwa watu pekee wenye mamlaka ya kufanya uteuzi wa viongozi wa muda ni sekretarieti ya klabu pekee.

Ameeleza kuwa hawautambui uongozi wa muda uliotangazwa na Baraza la Wadhamini Yanga kwa wao kama Baraza la Wazee.

Ikumbukwe siku chache zilizopita, Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini, George Mkuchika, alitangaza wajumbe wa muda wa Kamati ya Utendaji Yanga jambo ambalo Akilimali amepingana nalo vikali.

Tayari wajumbe hao wameshaanza kufanya kazi ikiwa ni kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Mei 5, 2019.




Post a Comment

0 Comments